Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo. |
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai anawatangazia Wananchi na Watumishi
wote kuwa dawati la malalamiko alilo anzisha litafanya kazi ya kupokea na
kutatua kero mbalimbali.
Ofisi ipo
wazi siku ya Jumanne na Alhamisi
saa tatu akamili asubuhi hadi saa tisa na nusu alasiri kweye ofisi ya kero
iliyopo katika Ukumbi wa Maktaba ya Hai.
Vile vile
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai atakuwa akipokea kero na
kutoa majibu yake kupitia Redio Boma Hai Fm siku
ya Ijumaa saa kumi na moja jioni kupitia kipindi cha Drive Home.
Aidha,mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai anapenda kuwahakiiishia kuwa uwepo wa usiri wa kero na taarifa zitakazo pokelewa.
Pia
mlalamikaji anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa njia ya barua na atume kwa
Mkurugenzi Mtendaji.
S.L.P 27,Hai
Fax:+255-272758441
Email:Mkurugenzihai@yahoo.com
Imetolea na:
Ofisi ya
Mkurugenzi MTENDAJI (W)
Hai.