Ametoa agizo
hilo alipo kuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mtakuja Kata ya Kia
Wilayani humo, mara baada ya kuendelea kupokea malalamiko toka kwa Wazee wanao
dai kuchangishwa fedha pasipo kutatuliwa shida zao kama walivyo ahidiwa.
“Binafsi
mimi naheshimu Wazee kwakuwa najua nami nitakuwa mzee ila nimekuwa nikipokea
malalamiko ofisini na katika vikao ninavyo fanya na wanakijiji maeneo tofauti
ndani ya wilaya,wazee wakimlalamikia katibu wa chama cha Wazee Shikinaufoo
Lema,kwa kuwachangisha fedha kila mara pasipo kuona changamoto zao zikitatuliwa
huku wakielezwa kuwa wakishindwa kuchangia watakosa huduma muhimu kwa
wazee”alisema byakanwa.
Byakanwa
amesema kuwa kipaumbela kwa Wazee toka serikalini nikuona kuwa wazee wanapewa
vitambulisho na kupewa matibabu bure kama sera ya serikali inavyo hitaji ili
kundi hilo liweze kupewa mahitaji muhimu kulingana na kazi na mchango wao kwa
serikali.
“Hicho chama
cha wazee Wilaya ya Hai kipo kibiashara zaidi kwani wakati naripoti kazini
walifika ofisini na kuhitaji ekari 30 za ardhi ambapo ombi hilo nililikataa
kwani siyo kipaumbele cha sera ya wazee.Wazee hao walirudi kwa mara ya pili
wakihitaji kiasi cha shilingi Bilioni 70 chini ya Katibu wao Lema.
Ameongeza
kuwa Chama hicho kimekuwa kikichangisha fedha vijijini kiasi cha shilingi 5000
kwa kila mzee pamoja na kutumia lugha ya ulaghai,kuwa endapo mzee atatoa kiasi
hicho cha fedha ataweza kuingizwa katika mpango wa TASAF,kupewa kipaumbele
katika mgao wa shilingi milioni 50 alizo ahidi Mh.rais pamoja na kupewa
Kitambulisho cha wazee.
Byakanwa
amesema kuwa hawezi kuzuia wazee kuwa na chama chao kama walivyo watu wengine
wenye vyama vya kusaidiana,lakini chama hicho kiwe kimekubaliana na tozo zinazo
tolewa ikiwa ni pamoja na idadi ya wanachama walio kubaliana na mashariti ya
katiba hiyo,jambo ambalo katibu huyo wa wazee hakufanya.
“kama vipo
vyama vya wazee katika vijiji vinatakiwa kufanya kazi kulingana na katiba
zilizo undwa kwenye vijiji vyao na siyo kupewa katiba ya Wilaya,hivyo kuanzia
leo ni marufuku kufanya michango kwa Wazee”alisema Byakanwa.
Byakanwa
ametoa siku tatu kwa katibu huyo wa wazee kufika ofisini na kutoa maelezo ya
kina dhidi ya malalamiko hayo,kwa kutoa maelezo ya fedha hizo zimetumika katika
shughuli zipi,ambapo katika kijiji hicho takribani wazee 40 wamechangishwa.
Hai kazi
ilijaribu kumtafuta kwa njia ya simu katibu huyo wa wazee ili kujibu tuhuma
hizo ila simu yake haikupatikana.