MAPAMBANO YA VIFO VYA MAMA NA MTOTO YAANZA MKOANI KILIMANJARO


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dr .Best Magoma,aliye simama akielezea dhumuni la semina hiyo,wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.





















Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Gelasius Byakanwa (Kushoto) Akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick katika semina hiyo.



Wauguzi wakuu wa hospitali za halmashauri za wilaya saba toka Mkoani Kilimanjaro wakifuatilia semina hiyo.

Hai-Kilimanjaro

WAUGUZI  wa kuu wa hosipitali za wilaya Mkoani Kilimanjaro wamekutana Wilayani Hai kwa lengo la kujadili na kupambana na vifo vya mama na mtoto ili kuweza kuvitokomeza ndani ya wilaya zote mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza katika semina hiyo Mganga mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro DR Best Magoma amesema kuwa bado mapambano yanahitajika kutokomeza  vifo vya mama na mtoto wakati na kabla ya kujifungua ilikuweza kuwa na watoto na akina mama waliohudumiwa vizuri kiafya na kuepukana na vifo hivyo.

Amesema kuwa katika utafiti uliofanywa wa kubaini vifo vya mama na mtoto Mkoani Kilimanjaro kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2014-2016 inaonyesha kuwa tatizo bado ni kubwa kwani 2014 kulikuwa na vifo 41 vilivyotokana na uzazi,2015 vifoo 56 na mwaka 2016 kulikuwa na vifo 47.

Magoma ameongeza kuwa kwa upande wa vifoo vya watoto wachanga  2014 vilikuwa 683 mwaka 2015 vilikuwa 604  na mwaka 2016 vikaongezeka na kufikia 631,jambo ambalo linahitaji ufumbuzi wa haraka ili kunusuru maisha ya mama na mtoto.

Ameongeza kuwa  licha ya huduma kuwa nzuri ya upatikanaji wa vifaa tiba na wataalamu wa afya bado tatizo hilo halija weza kutatulika na kumalizika kwa sababu mbalimbali hasa zinazo patikana ndani ya jamii,ikiwemo wajawazito kuchelewa kufika hosipitalini kwa wakati pamoja na baadhi kujifungulia nyumbani na inaposhindikana kukimbizwa hosipitali kwa kuchelewa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick amepongeza kuwepo kwa semia hiyo itakayo wawezesha kujadili masuala hayo kwa kina na muhafaka kuweza kupatikana ili kuondoa tatizo hilo la vifo vya mama na mtoto.

Amesema kuwa mbali na changamoto zinazo jitokeza katika kutoa huduma hizo,bado serikali inahakikisha kuwa vituo vya afya na hosipitali zina kuwa na wataalamu wa afya wa kutosha ikiwa ni pamoja na vifaa tiba vinavyo weza kunusuru maisha ya mama mjamzito.

“Nipende kuwa kumbusha na kuwaonya wajawazito kuacha kunywa pombe za kienyeji na kusahau kula vyakula vyenye kumjenga kiafya kwani baadhi ya wanywaji wapombe hizo pasipo kula wamekuwa wakipata utapia mlo na kuwafanya kushindwa kujifungua salama”
Alisema Sadick.


Semina hiyo itakayo dumu kwa siku tatu imehudhuriwa na wadau mbalimbali wa masula ya afya ya mama na mtoto, inalenga kuangalia njia za kutokomeza vifo vitokanavyo na kujifungua kwa akina pamoja na watoto ili kufanya mkoa wa Kilimanjaro kuondokana na idadi ya vifo hivyo.