Picha ya Gari walilokuwa wakisafiria Kutoka Rombo kurudi makwao mara baada ya kupata ajali eneo la Mwika Mawanjeni. |
From Media
Club Of Kilimanjaro.
Taarifa ya
msiba mkubwa kwa wanatasnia ya habari Mkoani Kilimanjaro na Taifa Kwa Ujumla.
Watu saba
wamekufa papo hapo katika ajali iliyo tokea eneo la Mwika Mawanjeni maarufu
kama “Baa mpya” akiwemo wanahabari wa magazeti ya serikali na Mwenyekiti wa
UVCCM wilaya ya Hai,Arnold Swai.
Swai na
wenzake walikuwa wakitokea katika sherehe ya miaka 40 ya CCM ambayo kwa Mkoa wa
Kilimanjaro ilifanyikia Wilayani Rombo.
Mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama na Mkuu wa wWlaya ya Rombo,Agnes Hokororo
alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo hilo na kuhusisha magari mawili pamoja
na pikipiki moja.
Wengine
waliyo fariki katika ajali hiyo ni pamoja na Anastazia Malaysia ambaye ni
Mwenyekiti wa UWT Tawi la Chuo kikuu Cha Ushirika Moshi(MOCU) Na mkazi wa
Shimbi,Rombo na Edwin Msele Katibu wa hamasa shirikisho la Vyuo vikuu Moshi
Mjini.
Wengine ni
Ally Mbaga(Mjumbe wa NEC) Wilaya ya Same na mkazi wa Mwanga,mwanamke ambaye
alikuwa katika bodaboda ambapo Fuso liligonga pikipiki hiyo na mtu mwingine
ambaye hajafahamika mara moja.
Hokororo
amesema kuwa majeruhi ni Mwnahabari Jackson Kimambo aliye kuwa anaendesha gari
aina ya Toyota Surf,ambapo hali yake inaendelea vizuri akipatiwa matibabu
hosipitali ya rufaa ya KCMC ambapo Miili ya marehemu wote imehifadhiwa chumba
cha kuhifadhia maiti katika hosipitali hiyo.
Taarifa za
awali kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kuwa gari
aina ya fuso lilifeli breki na kugonga gari hilo kwa nyuma kabla ya kuiparamia
na kuigonga pikipiki na kusababisha vifo hivyo.
Kamanda wa
Polisi Mkoani Kilimanjaro anatarajia kukutana na waandishi wa habari leo kuzungumzia tukio hilo.