Mwenyekiti wa Vijana CCM wilaya ya Hai Anorld Swai aliye shika mfuko wa saruji(kushoto) akikabidhi saruji mifuko 10 katika shule ya Msingi Uhuru. |
Hai-Kilimanjaro
UMMOJA wa
Vijana wa CCM wilaya ya Hai umewataka vijana wenzao kushiriki katika shughuli
za maendeleo bila kujali itikadi ya vyama vyao ili kuweza kuleta maendeleo
Kitaifa.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Vijana CCM
wilaya ya Hai Arnold Swai alipo kuwa akikabidhi mifuko 10 ya saruji katika
kuchangia ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Msingi Uhuru.
Amesema kuwa
ikiwa vijana ambao ndio nguvu kazi ya
Taifa watatambua nafasi zao nakuweka pembeni itikadi ya vyama vyao,maendeleo
yanaweza kupatikana kwa haraka kwani watapata nafasi ya kushirikiana kimawazo
na kiutendaji.
“Ifikie
mahali tuwe na umoja sisi vijana katika shughuliza kuleta maendeleo
yetu,tusitegemee wafadhili toka nje ya nchi kuja kutufadhili ilihali nguvu ya
kufanya kazi tunazo,hiyo itakuwa ni aibu.”Alisema Swai.
Awali
akizungumza na vijana waliokuwa wanajitolea kujenga vyumba hivyo vya madarasa
kwa kuelekeza nguvu zao katika kubeba mchanga na kujaza udongo,Katibu wa CCM
wilaya ya Hai Alan Kingazi amesema kuwa nivema mfano ulio oneshwa na vijana hao
kuigwa na vijana na vyama vingine ili kuharakisha shughuli za maendeleo ya
wilaya.
“Ikiwa mfano
huu utaendelea na kuigwa kwa vijana wa vyama vingine ni dhahiri kuwa umasikini
utapigwa vita kutokana na vijana kushiriki katika shughuli za kimaendeleo
katika masuala ya kielimu,afya,maji na barabara.”alisema Kingazi.