NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI AWATAKA WAFANYAKAZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI KUTIMIZA WAJIBU WAO ILI KUEPUKA KUTUMBULIWA


Naibu Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jaffo akipokea maelekezo kutoka kwa Mtaalamu wa mionzi.
Hai-Kilimanjaro.
NAIBU waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Suleima Jaffo amewataka wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai kuwa waadilifu na kutimiza wajibu wao ili kuendana na kasi ya Mheshimiwa  rais John Pombe Magufuli .

Ameyasema hayo leo katika ziara yake Mkoani Kilimanjaro wakati alipo tembelea Halmasahuri hiyo kukagua jengo la mionzi katika hospitali ya wilaya pamoja na kuzungumza  na wafanyakazi wa halmashauri hiyo.

Jaffo amebainisha kuwa wafanyakazi wa serikali wanapaswa kutimiza majukumu yao na kuhudumia wananchi kwa wakati ili kuweza kuondoa lawama zinazo lalamikiwa na wananchi wanao hitaji huduma yao.

“Niwaombe sana nyie wakuu wa idara na watendaji wenu,muhudumie wananchi kwa kiwango kinacho hitajika ili kuweza kuondoa minong’ono kwanza ndani ya ofisi zenu na nje ya ofisi kwa watu mnao wahudumia”alisema Jafo.

Jaffo ameipongeza halmashauri hiyo kutokana na madiwani wa halmashuri kuweza kushirikiana na wafanyakazi wa ndani pamoja na  viongozi wake katika masuala muhimu ya kuchochea maendeleo ndani ya halmashauri sambamba na kushauriana katika njia yenye kuleta neema kwa wananchi.

“Nijambo la kupendeza kuona kuwa mnaweka itikadi yenu ya vyama pembeni katika suala la maendeleo kwa kuamua kwa busara ikiwa ni pamoja na kuelekezana hadi kufikia hatu za maendeleo kila kukicha wilaya ya Hai inaonekana kuoendeza”alisema Jafo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Gasper Byakanwa amemtaka Naibu Waziri kufika tena katika wilaya hiyo ilio kuweza kujionea utekelezaji wa mambo ya kimaendeleo waliyo ahidi kuyamaliza ili miradi hiyo iweze kuwa nufaisha wananchi.

“Nikuombe Naibu Waziri kututembelea mara nyingi uwezavyo ili kuweza kujiridhisha na mipango tuliyo kueleza na kujionea ikifanya kazi kwa kiwango kinacho hitajika.”Alisema Byakanwa.


Naibu Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jaffo katikati akiweka saini katika kitabu cha wageni katika hospitali ya Wilaya ya Hai




Jengo la upasuaji kwa Wanawake na Wanaume katika Hospitali ya Wilaya ya Hai  linalo tarajiwa kukamilika mwaka huu na kuanza huduma rasmi.



Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wakati akitoa hotuba yake fupi.\
picha zote na Haikaziblog.