Baadhi ya wananchi wenye malalamiko na migogoro katika maeno yao wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya katika kikao hicho. Hai-Kilimanjaro |
MKUU wa
Wilaya ya Hai Gelasius Gasper Byakanwa ametaja orodha ya wananchi walioshindwa
kuendeleza viwanja vyao walivyo nunua sambamba na viwanja venye mgogoro ili kuweza
kutatua migogoro na kupelekea mji wa Bomangombe kukaa katika hali nzuri.
Ametaja orodha
hiyo leo wakati wa kikao cha muendelezo wa kusikiliza migogoro ya ardhi alio
uanzisha hivi karibuni ulio wakutanisha wananchi wenye malalamiko ya viwanja
vyao pamoja na maafisa ardhi wa Wilaya.
Byakanwa
amesema kuwa amekuwa akipokea malalamiko toka kwa wananchi wa Hai mjini na nje
ya mji mdogo wa Bomang’ombe badhi yao wakiwa wakweli na wengine siyo wa kweli walio
uziwa kiwanja au viwanja vyao bila utaratibu maalumu wa kulipwa fidia jambo
linalo pelekea makazi yao kushindwa kuendelezwa kama inavyo hitajika.
“Niwe muwazi
kuwa kuna baaadhi ya viwanja vilivyo onekana kuuzwa mara mbili mbili na kuleta
usumbufu unao weza kuibua migogoro na chuki zisizo hitajika na kwa kuangalia
hilo ni katika ofisi ya ardhi ndio walio fanya mchezo huo,hivyo nawataka
kutatua na kugawa maeneo hayo kwa utaratibu unao kubalika”alisema Byakanwa.
Byakanwa
ameongeza kuwa kwa wale walio kwisha kununua
maeneo au kupewa maeneo na kushindwa kuyaendeleza maeneo hayo kuwa,
maeoneo hayo yata chukuliwa na kupewa watu wenye uwezo wa kuyaendeleza ili
kuruhusu Mji kukua kwa mpangilio unao hitajika.
Kwa upande
wake Afisa ardhi wa Wilaya Poesent Majumba amekiri kuwepo kwa wananchi wanao
lalamika maeneo yao kuchukuliwa au kuuzwa pasipo kujua,hivyo kuahidi kutatua
matatizo hayo ili haki zao ziweze kupatika kwa wakati.
“Nipende
kusema kuwa kwa kikao hiki cha leo na vitakavyo endelea kufanyika ,ni wazi kuwa
tutajitahidi kumaliza matatizo hayo ikiwa ni sambamba na kugawa maeneo kwa watu
wanaostahili pamoja na kurudisha maeneo ya watu walio shindwa kuendeleza maeneo
yao”alisema Majumba.
Naye Erasto
Massawe mkazi wa Bomang’ombe anaye lalamika kiwanja cha familia yao kuchukuliwa
pasipo kuwa na utaratibu maalumu ameshukuru kuwepo kwa utaratibu huo mpya wa
Mkuu wa Wilaya hiyo kukaa na wananchi wenye malalamiko na kuwasikiliza ili
kuweza kutafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo.
“Kwakweli
mimi nishukuru kwa utaratibu huu sijawahi ona Mkuu wa Wilaya aliye kaa na
wananchi kuwasikiliza na kutoa ushauri,nadhani huu ni utaratibu mzuri wenye
maono ya kuona migogoro ya ardhi ina malizika”alisema Massawe.
Picha na Haikaziblog.